Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernet Mangu akimpa mkono mshindi wa Kwanza wa Riadha ya Half May Day Marathon katika kundi la Wanaume,Alphonce Felix wa Club ya Holili,Kilimanjaro yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Boa Bank Ammish Owusu, mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
.Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa Kwanza wa Riadha ya Half May Day Marathon katika kundi la wanawake,Natalie Elisante Arusha) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Suleiman Kova ,mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa Pili wa Riadha ya Half May Day Marathon katika kundi la wanaume ,Joseph Panga (Arusha) yaliyofanyika leo katika viwanja Polisi Ostebay jijini Dar es Salaam wanaoshuhudia ni ,Mkurugenzi wa Benki ya Boa,Ammish Owusu .
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu amesema michezo inajenga ukakamavu wa mwili hivyo kwa washiriki wa may day marathon wamefanyoa afya.
Mangu ameyasema aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati mashindano ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam ,aliwapongeza washindi na kutaka waongeze juhudi ili waweze kufika mbali katika mchezo wa riadha. Washindi wa May Marathon wamepongeza waandaji wa mashindano hayo kwani yanaongeza chachu ya kupenda mchezo huo.
Washindi hao wameyasema hayo katika mashindano ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterba jijini Dar es Salaam ,wamesema kuwa mashindano hayo yameamsha kupenda mchezo wa riadha kuendelea kupendwa.
Akizungumza na mshindi wa kwanza katika upande wa wanaume ,Alphonce Felix amesema ameshinda katika mashindano hayo kwani alijituma kutokana na mazoezi ya mara kwa mara na kuwataka watu wengine kushiriki mchezo huo kutokana na kujenga afya zao.
Amesema riadha ni mchezo mmoja mzuri kutokana na utaratibu kujpangia mazoezi kwa ni riadhia ni ajira kama michezo mingine.
Mshindi wa Kwanza kwa upande wa Wanawake ,Natalie Elisante (Arusha)amesema amewataka wasichana kushiriki katika riadha mbalimbali kwani wasichana na wanawake wanaoshiriki mchezo huo ni wachache ikilinganishwa na idadi yetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...