Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ameanza rasmi ziara ya kikazi katika kanda ya kusini ambapo ameanza ziara hiyo kwa kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika wilaya ya kitanesco ya Makambako, Mhandisi Abdulrahman Nyenye, amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo ni kielelezo cha utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili inayotekelezwa na TANESCO kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akibonyeza kitufe kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto) akiangalia kikundi cha utamaduni cha mkoani Njombe mara baada ya kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mhe. Deo Sanga.
Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mhe. Deo Sanga (wa pili kulia) akieleza hali ya nishati katika Jimbo lake mara baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati) kuwasili katika Ofisi za Tanesco, wilaya ya kitanesco ya Makambako mkoani Njombe akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo cha kufua umeme mkoani Ruvuma. Wa pili kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika wilaya ya kitanesco ya Makambako, Mhandisi Abdulrahman Nyenye.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye shati la mistari) akiangalia jinsi wateja wanavyohudumiwa katika ofisi za Tanesco, Makambako, mkoani Njombe. Naibu Waziri alitembelea ofisi hizo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo cha kufua umeme mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...