Mh. Rose Kirigini mbunge wa viti maalumu wa CCM na mkuu wa wilaya ya
Maswa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya ujenzi amemuumbua
Mh.Mkosamali aliyesema kuwa ilani ya CCM haijatekeleza ujenzi wa
barabara kwa kiwango cha lami inayotoka Mwigumbi - Maswa - Bariadi -
Lamadi, Kolandoto - Lalago na Meatu Mjini.
Alisema kwamba mkandarasi
yuko site na tayari ameanza kazi za ujenzi sehemu ya Mwigumbi - Maswa
na Ujenzi unaendelea kwa Bariadi – Lamadi (km 71.8) . Aidha Barabara
ya Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala – Oldeani Jct (km 328),
Mkataba umesainiwa na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina
imeanza Julai, 2014 na zinatarajiwa kukamilika Machi, 2016.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...