MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ambayo ndio inaandaa matamasha ya Pasaka na Krismasi, Alex Msama amekemea waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania kufanya kazi ya Mungu na kuachana na siasa ambazo zinawaondoa kwenye uinjilishaji. 

Msama ameyasema hayo wakati tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na urais unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Msama anasema karipio hilo linawahusu pia viongozi wa dini wakiwamo Wachungaji na Maaskofu  ambao wanaonesha nia ya kutaka kuwania uongozi wa kisiasa katika nafasi hizo tatu.Sababu za Msama kukemea waimbaji wa Injili kujihusisha na Wanasiasa wakiwemo wagombea urais, kuna baadhi ya waimbaji wametunga nyimbo za ‘kuwatukuza’ wagombea urais wakati wao wanatakiwa muda wote kumtukuza Mungu na si binaadam wenzao.

“Waimbaji tunatoka katika mstari, kwani Mungu anawategemea kufikisha ujembe wake kwa lengo la kuachana na machukizo ambazo yanapoteza mwelekeo wa jamii mbalimbali ambazo zinahitaji maono ya Wainjilisti,” alisema Msama na kuongeza. “Waimbaji ambao ninashirikiana nao katika kufikisha huduma ya neno la Mungu, nashangaa wanatoka katika mstari nawaomba wamrudie Mungu kwani wanapotea wakiwatumikia mabwana wengine.”  Alisema.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...