Mwenyekiti wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi watano kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyeopo Madarakani kutaka kuongeza muda wake.

Akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhula wa Tatu.

Amezungumzia juu ya waandamanaji  baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.

Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.

Pia ameiomba Jumuiya ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea kwa sasa  Nchini Burundi ambapo jumuiya hiyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.

Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo 

Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa Muhula wake ni Haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo.

 Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.

Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.

Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu. 
 Mwenyekiti wa Vuguvugu kutoka nchini Burundi Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea na waandishi wa Habari Usiku huu Serena Hotel Dar.
 Dr. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari usiku Huu. 
Kikao Kikiwa kinaendelea usiku Huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2015

    Amani Burundi ni muhimu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2015

    Tusome alama za nyakati.Rais aliyeko madarakani aachie madaraka kama muongo wake umekwusha.HIVI KWANINI WAAFRIKA TUNAPENDA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA.TUACHE HIYO TABIA .TUUJIFUNZE KWA WENZETU WANAKUBALI KUACHIA MADARAKA NA PIA WANAKUBALI KUSHIƑDWA PIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...