Na Teresia Mhagama
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amezindua mradi wa umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma ambapo jumla ya nyumba 100 zimeshafaidika kwa kuunganishwa na huduma ya umeme.
Akiwa ameambatana na mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama, Naibu waziri Mwijage, alitembelea na kukagua mitambo pamoja na mkondo wa maji yanayozalisha umeme huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (kulia kwa Naibu Waziri) wakiwa katika eneo ambalo limejengwa mfereji unaopeleka maji katika mitambo ya kuzalisha umeme wa kiasi cha kilowati 40. Mradi huo umebuniwa na wananchi katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (katikati) ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho, wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili kulia) akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea chumba chenye mitambo ya kuzalisha umeme wa kiasi cha kilowati 40 katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama , wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Nyasa, Fredy Mahobe na wa kwanza kushoto ni Afisa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Emmanuel Yesaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...