Na Faustine Ruta,
Bukoba
Katika kutengeneza ajira kwa vijana na kuuendeleza mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali na ndani ya mkoa Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Nassor Mnabila aliamua kuanzisha timu ya mpira ya mkoa wa Kagera. 
Madhumuni ya kuanzisha timu hiyo ni kuuleta mkoa wa Kagera pamoja, kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya michezo aidha kuutangaza mkoa nje na ndani ya nchi kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya mkoa wetu wa Kagera. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila mara baada ya kuanzisha timu hiyo ambayo kwa sasa inajulikana kama RAS Kagera Football Club na kuiwezesha kushiriki ligi daraja la nne na daraja la tatu na kufuzu kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda katika kituo cha Mbulu mkoani Manyara . 
Kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Mkoa wa Kagera hasa wapenda michezo na maendeleo ya mkoa wa wameweza kuichangia timu hiyo ili kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda na kama ikifuzu itaweza kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa. 

Ushiriki wa timu hiyo unahitaji michango ya wadau kwani ni timu ya mkoa inayouwakilisha mkoa wa Kagera wadau walioweza kuichangia timu hiyo ni pamoja na Wadau wa maendeleo toka Dar es Salaam pamoja na Wadau wa maendeleo waliopo mkoani hapa. 

Aidha wanasiasa hawakubaki nyuma ambapo Mbunge wa Bukoba Vijiji Mhe. Jasson Rweikiza naye ameichangia kiasi cha shilingi 300,000/- na Mbunge wa Meleba Kaskazini Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Charles Mwijage leo tarehe 20/05/2015 ameichangia timu hiyo shilingi 1,000,000/- 
Wadau wote wa maendeleo wa mkoa wa Kagera mnaombwa kumuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ili kufanikisha adhima yake ya kuuendeleza mkoa huu hasa katika sekta ya michezo. Aidha kwa wote wenye nia na mapenzi mema ya kuichangia timu hiyo wananweza kuonana na Mwenyekiti wa kamati ya muda Bw. Seif Hssein Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...