Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi Nchini(NEC),inatarajia kuchunguza
mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi na kuyagawa kwa ajili ya uchaguzi wa
Wabunge unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti
wa NEC,Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokutana na viongozi wa Vyama vya
Siasa kujadili masuala mbalimbali ya Tume katika kuelekea uchaguzi Mkuu.
Amesema ugawaji wa Majimbo,Tume imezingatia
vigezo mbalimbali ikiwemo idadi ya watu,upatikanaji wa mawasiliano hali ya
kijiografia na vigezo vingine kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Rais na
Wabunge ya mwaka 2010.
Jaji Lubuva amesema ugawaji wa majimbo hufanyika
kila baada ya miaka 10 na ugawaji huo utafanywa kabla ya Oktoba na hii
inatokana na kuongezeka kwa idadi ya watu katika majimbo na kuona kuna umuhimu
wa kugawa majimbo kwa mujibu wa sheria.
Aidha amesema ugawaji wa majimbo sio kwa kuangalia
idadi ya watu,bali upatikanaji wa mawasiliano inayojumuisha
miundombinu,simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi
atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika.
Lubuva amesema kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kama
ulivyokuwa umepangwa kutokana na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura linaendelea katika mikoa iliyoainishwa.
Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva akizungumza katika
Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali
kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud
Hamid.
Mwenyekiti wa Taifa Chama cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba akichangia maada katika Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali
kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP),Nancy Mrikaria akitoa ufafanuzi juu ya viti maalumu Bungeni katika Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali
kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...