Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.

Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni vizur wametoa na wameweka waz jambo hili

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2015

    Puliza kipyengaaaaa tuwamwage.....yaani mzigo ulivyotuchosha we acha tu.....yaani wangejua wasinge ingiza timu aibuuuu.......

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2015

    Hasira zetu dhidi ya hali duni ya wananchi wengi mijini Na vijijini tuimalize siku hiyo kwa kuwachagua viongozi wenye sera endelevu Na ukombozi Na wenye ahadi zinazoweza tekelezeka,hii Ni nafasi pekee ndugu zangu kwa kuwaadhibu kwa kutowachagua wote tuliowapa dhamana ya miaka kadhaa Na kutudanganya kwa ahadi hewa,tunataka kiongozi anaesimamia sera za jimbo au mkoa kwa kasi kubwa ya maendeleo.tuwaoneshe kuwa sisi ndio wenye nchi Na Wao Ni wawakilishi wetu Tu.tuepuke kufanywa Kama karai la kujengea Lina thamani Tu pale ujenzi unapoendelea Na ujenzi ukiisha karai halina kazi.wananchi tuache ushabiki wa vyama tuchague kiongozi atakaetuletea mabadiliko Na unafuu wa maisha.nchi nyingi afrika Na dunia zimeonesha kuwa wanataka mabadiliko nasi pia tunaweza kuwa Na maisha yenye nafuu Na yalo bora.tunatala kiongozi atakaetuhakikishia elimu bora,tunapata matibabu kwa urahisi Na nafuu,umeme nafuu,bei ya chakula kwa gharama nafuu Na usalama wetu Na Mali zetu,tunahitaji kiongozi mwenye kuujua utawala bora Na usimamizi wa sheria hasa ktk mifumo ya mahakama Na atakaeweza kutuondolea kero zote zinazotuzunguka .Ahsanteni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...