Familia ya Bw. Uwesu Y.Mssumi wa Mbezi Beach Dar es Salaam inatoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada ya hali na mali wakati na maobolezo na hatimaye mazishi ya mke wake mpendwa Mwalimu Hidaya U. Mssumi ( mama ya Fatuma, Mwanana, Bibie na Mariam) kilichotokea tarehe 27 April na kuzikwa tarehe 28 April, 2015.
Shukurani za pekee ziwafikie wanajumuiya wa masjid Akram, Taqwa, Noor na Fauz Mbezi Beach, masjid Maamur- Upanga, Dr. Halid Gongoro, Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani na wilaya ya Rufiji, Menejiment za kampuni ya Export Trading Group, Mgodi wa Acacia North Mara, Chuo Kikuu Dodoma na Takukuru Mkoa Manyara bila kuwasahau wanafunzi waliomaliza shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988.
Haitakuwa rahisi kuwataja wote waliotusaidia na kushirikiana nasi ila kwa ujumla wenu tunawashukuru sana kwa kutupa faraja wakati wa kipindi hiki kigumu.
Tunawakaribisha na tunaomba tushirikiane nanyi katika arobanini ( Duah) ya kumwombea marehemu itakayofanyika tarehe 6 Juni, 2015 baada ya swala ya Adhururi ( saa saba mchana) . Duah hii itafanyika nyumbani Mbezi Beach kitalu J plot na 229/30 mtaa wa Mufindi (off Mwai Kibaki Road)
Inna Lilah waina Lilah Rajuhun.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...