Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (kulia) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.
Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya (chini) kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.
Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015
Hongera Balozi na Yayha kwa uteuzi huu.
ReplyDeleteHongereni sana Mama Mulamula na Bwana Yahaya kwa uteuzi huu!
ReplyDeletekiukweli mna bahati marekani kuwa na balozi kama huyo anayejitkeza hata kwenye mikusanyiko ya watanzania...ila wenzenu huku Canada kikwete anakosea mabalozi tokakamtoa khalage kumekuwa kimya ila nasikia kuna balozi mwingine kaja wenda akawa mzuri.ni shidaa
ReplyDelete