Rais
wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua
Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani
kuanzia Jumamosi iliyopita, Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam,
leo, Alhamisi, Aprili 30, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.
Taarifa
hiyo imewataja wajaji hao kuwa ni Jaji
Augustine Gherabast Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha,
ambao wote wamekuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa
Novemba 28, 2006.
Kabla
ya uteuzi wake, Jaji Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara,
Mahakama Kuu, Dar Es Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili
wa Mahakama ya Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.
Aliajiriwa
kama Hakimu Mkazi Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada
ya Sheria mwaka 1986.
Naye
Jaji Mugasha, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam.
Alikuwa Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu
2009 hadi alipohamishiwa Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.
Aliajiriwa
kama Wakili wa Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo
huo, 1983.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30
April, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...