Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band almaarufu kama FFU-Ughaibuni yenye maskani yeke nchini Ujerumani,siku ya jumamosi 30 Mei 2015 bendi hiyo italitingisha hekalu la Uebersee Museum mjini Bremen,kuanzia Saa moja Usiku hadi kumekucha.
Onyesho hilo la usiku usiokwisha limeandaliwa na utawala wa hekalu hilo la makumbusho la Uebersee Museum,ambapo utawala huo umeiomba bendi ya Ngoma Africa band kwenda kutumbuiza,kwa kuwa bendi hiyo ilitumbuiza mwaka 2013 na kuvunja rekodi ya kuwavuta washabiki wengi kuliko bendi yeyote katika historia ya matamasha yafanyikao katika hekalu hilo.
Ngoma Africa band inayoongozwa na kamanda Ras Makunja ni bendi pekee ya kiafrika yenye mvuto mkubwa barani ulaya,na washabiki wake wameipachika majina mengi ya kiusanii kama vile FFU-Ughaibuni,Viumbe wa ajabu ANUNNAKI Alien's (himaya ya mazimwi wa Anunnaki), pia maarufu kwa majina kama Mzimu wa Muziki,na "Watoto wa Mbwa" .
Ngoma Africa band pia inatajiri wa wanamuziki wenye vipaji vya hali ya juu wakiwemo yule mpiga solo mahiri Afande Chris Bakottesa aka Afande Chris-B, Sanjint major Jo jo Sousa, wanamuziki chipukizi wengi walizalishwa na bendi hiyo ambayo inawanamuziki kumi.

Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 na kiongozi wa bendi hiyo ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo nyingi za bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja.
unaweza kuwasikiiza FFU
unaweza kujumuika nao pia at ngoma4u@gmail.com
Jina la WATOTO WA MBWA walipewa na mgombea urais wa chama kimoja cha upinzani 2010 kwa kuwa walimbwakia kwa kupitia kituo kimoja cha redio,Mzee yule hakuwavumilia akamua kuwapa jina la WATOTO WA MBWA
ReplyDeleteSi mchezo ffu wanatisha wanapotuachaga midomo wazi ni yale madongo katika nyimbo zao
ReplyDeleteFFU -ughaibuni aka wazee wa gwaride jamaa awapendagi kulemba wao ni mbele kwa mbele tu
ReplyDeleteKikosi kazi chini ya kamanda mkuu aliyeipindia akili kazi yake
ReplyDelete