MFUKO
wa Pensheni wa PPF, umepewa cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa
wananchi (ISO) baada ya kukidhi mashariti na vigezo.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio alitoa taarifa hiyo leo Ijumaa na kusema kuwa walipewa tangu Machi 28, mwaka
huu.
Alisema
wamepewa cheti chenye namba 9001:2008 na kuanzia mwezi Mei, mwaka huu huduma za
PPF zinaza kutambulika kimataifa.
“ISO
walikuja nchini wakatukagua wakalidhika na viwango vya huduma zetu tunazotoa na
wakatupatia cheti cha ubora,” alisema Erio.
Alisema
kwa sasa wanachma wa PPF wategemee kupata huduma bora pamoja na uwajibikaji
ulio bora.
Alisema
kila baada ya miezi sita ISO watakuwa wanatembelea PPF na kukagua kama huduma
bora bado zinatolewa, na kila baada ya miaka mitatu PPF watatakiwa ku-renew
maombi ya ISO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
William Erio (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa
wananchi (ISO) walichokipata baada ya kukidhi mashariti na vigezo
![]() |
Mameneja wa PPF, na waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio juu ya tuzo hiyo |
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
William Erio (katikati), Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Julius Mganga
(kushoto) na Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga (risk management), Ufoo Swai
wakionyesha cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa wananchi (ISO) wakati
wa mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam
leo Ijumaa Mei 29,2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...