Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa
Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge
lao mjini Dodoma.
.Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Rais wa Msumbiji
Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa Msumbiji alipowasili katika makao
makuu ya CCM m.Jakayajini Dodoma na kuzungumza na viongozi waandamizi .Kushoto
ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania
Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika
viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea
heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma
akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini
kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia
(Picha na Freddy Maro)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...