Domain ni Nini?
 Ikiwa kuna mtu anataka kutembelea tovuti/website yako (kama wewe ulivyotembelea website hii) atahitaji kutumia domain yako au kwa kuiandika moja kwa moja au kupitia link kutoka kwenye search engine ili kuweza kuiona.
 Kompyuta huwasiliana kwa kutumia namba zinazoitwa anwani ya IP (IP Address). Hii  ni sawa na unavyo tumia namba ya simu fulani kuwasiliana na fulani. Jina la domain katika mtandao ni kama jina linaloendana na namba husika za simu katika simu yako.

Badala ya kukariri namba za simu za watu wote, unaweka namba na jina kwenye simu yako maana majina unaweza kuyakumbuka kirahisi. Vivyo hivyo, badala ya kukariri IP address (ambazo) ni namba kwenye mfumo huu 123.456.789.123/ wateja wako watalijua tu jina lako/domain ambayo yaweza kuwa jinalako.co.tz  

Jinsi ya kupata ‘domain name’
Katika kufanya kuwa rahisi kwa wewe kuandikisha domain yako, Tanzania Network Information Centre (tzNIC)  wamekupa njia mbili mbadala: -
Njia ya kwanza ambayo ni rahisi tzNIC wamewapa vibali zaidi ya wasajili 20  nchi nzima ambao wanauwezo wa kukusaidia wewe kuandikisha domain yako kwa bei nafuu kabisa ya TZS 25,000 tu au USD 30 tu. 
Na zaidi sana kwa kutumia hao wasajili wenye vibali utapata pia huduma ya hiyo domain yako kuwa hosted ambayo kwa lugha rahisi ni eneo katika ulimwengu wa digitali unaloweza kufanyia lolote ikiwemo pamoja na kuuza bidhaa zako na kutuma na kupokea email.

Hawa wasajili waliopewa vibali na tzNIC  pia watakupa huduma ya kusimamia website yako ili usiweze kupata tatizo lolote kwa kipindi chote cha matumizi yake. Tanzania Network Information Centre (tzNIC) pia wameweka huduma ya kujisajili na tzNIC moja kwa moja ingawa hawa shauri ufanye hivyo.

Chaguo hili linahitaji kidogo kujua maarifa ya kiufundi katika field ya digitali. Ili kuwa na haki ya kujiandikisha moja kwa moja na tzNIC lazima kutoa anwani Itifaki ya Internet yani Internet Protocol yenye name servers mbili ambazo inabidi ziwe zimeunganishwa kwenye mtandao kwa kudumu pamoja na malipo ya TZS45,000.

Wahi mapema kusajili jina la kampuni au biashara yako au hata kama ni mtu binafsi kabla mpinzani wako kibiashara hajasajili yeye. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea kurasa za TzNic hapa chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...