Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu), George Mkuchika akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa uwazi na kusikilizana kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali barani Afrika mkutano uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene akichangia  kwa upande wa serikali kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu, wakati wa mkutano wa Uwazi na usikivu katika mambo ya uchumi serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali  katika bara la Afrika.
 Mkurugezi wa kampuni ya Compass Communications Ltd,  Maria Sarungi akizungumza katika mkutano wa Uwazi na Usikivu  uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika, mkutano hup umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugeni Mkuu wa TWAWEZA Aidani Eyakuza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika kufunga mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wadau wa mkutano kutoka nchi mbalimbali  za Barani Afrika walihudhuria  mkutano uliofanyika  katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Serikali na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali  Barani Afrika zimetakiwa kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya  uendeshaji wa mambo yake kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi.

 Hayo yamesemwa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali Barani  Afrika  kutoka serikalini na Taasisi zisizo za kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.

Mkuchika amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema kufanikisha malengo ya nchi.

Pia kwa upande wa serikali amesema kuwa  serikali ikiweka mambo yake kwa uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu nini kinaendelea katika nchi husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...