Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akisoma taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi
dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi kuhusu
kuhusika kwake na kashfa ya Escrow na ile ya tume ya uchunguzi wa malalamiko yaliyotokana
na utekelezaji wa operesheni tokomeza mapema hii leo jijini Dar es Salaam , kulia niMwandishi
wa Habari Msaidizi wa Rais Bi. Premi Kibanga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue wakati akisoma taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya aliyekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi kuhusu kuhusika kwake na kashfa ya
Escrow na ile ya tume ya uchunguzi wa malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa operesheni
tokomeza.
Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO.
Mh Katibu Mkuu kama watu wote waliokuwa wanachunguzwa HAWAHUSIKI je ni nani hasa anayehusika na upotevu wa hayo mabilioni na mauaji ya raia wasio na hatia kwenye hiyo operesheni tokomeza?
ReplyDeleteJamani tukumbuke kuwa kuna Mungu atakae tuhukumu siku ya mwisho kwa kutokuwa watu wa HAKI duniani. Yeye Mungu ndie aonaye maumivu na vilio vya wa-tz maskini wasiotendewa haki.
Mama Jesca