Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendeshwa na kampuni ya Proin Promotion linalolenga kuinua vipaji kwa vijana ikiwa ni katika kuwatengenezea mazingira ya ajira katika maisha yao Nchi nzima kikanda lionekana kuwa msaada kwa vijana wengi waliokuwa wakijitokeza kushiriki mashindano hayo katika mikoa mbalimbali tulikopita.
Shindano la ya Tanzania Movie Talents msimu wa pili 2015 lilioanza mwezi Aprili kikanda kwa kuanza na kanda ya ziwa mwanza, Kanda ya kaskazini Arusha,Kanda ya kati Dodoma na kisha kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya limekamilika kwa siku ya jana kupatikana washindi watatu na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano kila mmoja kati ya washiriki mia tatu waliojitokeza kushindana
Jana jioni Jijini Mbeya Soko Matola Mkapa Conference Center ndipo mashindano hayo yalipofanyika na kuhudhuliwa na vijana kutoka wiraya zote za mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani kama Iringa na mikoa mingine ya jirani.
Washindi hao watatu watakwenda kuungana na wenzao wa kutoka kanda zote nchini kwa kuingia kwenye nyumba ya TMT wakifundishwa sanaa na waalimu mbali mbali kutoka Chuo kikuu Mlimani,kisha kuwepo na mtoano wa kila wiki ilikubaki washiriki kumi na mwisho kupata mmoja atakayeibuka na shilling Milioni Hamsini za kitanzani,hao kumi watakao baki wataigiza movie ya pamoja ikiwa ni katika kuwatambulisha katika tasni ya sanaa nchini ili iwe ajira kwako.
Baada ya kutoka Jijini Mbeya ni Mtwara tarehe 26 na 27 mwezi huu kisha Dar es salaam 5-7 mwezi wa 6,kwa taraifa zaidi tazama ITV na sikiliza Redio one au redio za mkoa husika kujua taharifa zaidi za mahala na muda.
TMT2015 #mpakakieleweke
Meza ya kufanya usajili kabla ya kuingia ndani kuonesha kipaji chako kwa majaji wa TMT |
Foleni ya wasanii wa Mkoa wa mbeya waliojitokeza kuchukua form kujisajili katika Shindano hilo |
Foleni ya wasanii wa Mkoa wa mbeya waliojitokeza kuchukua form kujisajili katika Shindano hilo |
Wasanii wa Mkoa wa Mbeya walipokuwa wakipewa maelezo na kuuliza maswali kuhusu shindano la TMT. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...