Katika
kukabiliana na vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino),leo jeshi la jadi sungusungu katika
halmashauri
ya manispaa ya Shinyanga limekabidhiwa pikipiki yenye thamani ya
shilingi milioni moja, laki 6 na elfu 50 kwa ajili ya kuhimarisha ulinzi
na usalama kwenye maeneo yao.
Zoezi la makabidhiano limefanyika katika
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa
wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi
na usalama katika wilaya hiyo.
Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na
kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga, James Deshi.Pichani katikati
ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi
ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro
ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu
wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.
Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki
hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na
kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo
hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika
kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
Matiro
alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki kwa jeshi la sungusungu
katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini
Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na viongozi wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga
Viongozi
wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka
na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la
sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...