
Jumuiya inapenda kuwatangazia watanzania wa eneo la 'Washington State' na maeneo ya Idaho, Oregon, kujiandikisha kwa wingi wale wote wenye kuhitaji kuomba PASSPORT MPYA YA TANZANIA kama ifuatavyo:
Siku ya mwisho kujiandikisha ni Tarehe 5/6/2015 (June 5th, 2015)
Siku ya kuonana na Ofisa wa Uhamiaji kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa ajili ya maombi hayo ni Tarehe 26/6/2015 - Taarifa ya pahala itatolewa rasmi..
Tafadhali wasiliana na wafuatao kujiandikisha rasmi:
Emil Muta - Mwenyekiti Tanzaseattle - simu - 206 291 8835
Haji Rajab Haji - Katibu Tanzaseattle - 206 302 9404
Au
Unaweza kutuma barua pepe (email) - Tanzaseattle @gmail.com
-
Ahsanteni sana.
Mkuu wa Kitengo cha Habari - Tanzaseattle.
A. DOLA - aka (Mayor of Seattle) - 206 422 3050.
Naomba nieleze au niweke sawa kuhusu hili,mnaposema passport passport mpya za Tanzania mnamaanisha nn ? mimi ni Afisa wa Uhamiaji,japokua sio msemaji wa idara ila napenda kuelezea mana ni watu wengi wamekua na imani kuwa Tanzania wanatoa passport mpya. Ukweli ni kwamba hakuna passport mpya na wala serikali haijawazan kubadilisha pasi za kusafiria. Kinachofanyika kwa kuwa hizi passport zilianza kutumia miaka kumi iliopita sasa ni wakati wa kubadilisha kwani ukomo wa pasi ni miaka 10. Unapata pasi nyengine lakini ni zile zile na muundo ule ule. Tuwafahamishe watu vyema ili kusitokee siitafahamu isiotakiwa.
ReplyDeleteTumejaza kila kitu kuomba hizo pass na kutiwa sign ubalozini na bahasha kuwa imefungwa na ubalozi, tayari kuomba pass.
ReplyDeleteZikifika Tanzania wanaomba vyeti original vya anae omba na cheti cha mzazi.
Wakati hivi vitu vimeshaangaliwa na officer wa migration ktk ubalozi.
Napia mbona wenzetu wa Uganda na Kenya hili si jambo kubwa wao wana pata pass tuu katika balozi zao hawana haja ya kupeleka ktk nchi zao.
Kwani nn kila kitu cha Tanzania nishida.
mchangiaji hapo juu napenda kukuelewesha kuwa kila nchi na sheria zake na taratibu zake. tanzania ni nchi huru na hailazimiki kufuata mfumo wa nchi yoyote ile duniani. kwamba kenya na uganda wanagawa passport kama pipi haina maana na sisituige mfumo huo.
ReplyDeletesheria ya tanzania inatambua kuwa passport ni utambulisho wa uraia. hivyo mtu akiwa na passport ya tanzania ni raia wa tanzania. katika hali tuliyonayo ambapo tumezungukwa na wakimbizi, wahamiaji haramu na wazamiaji, kutoa passport kiholela sio jambo la busara hata kidogo.
hivyo uhakiki wa vyeti ni muhimu kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo. kinyume chake watoto wetu na wajukuu wetu watakuja kutuhukumu kwa uzembe wetu.
shukran.
We Anonymous wa 3 vipi? Mbona hueleweki? Mbona jamaa wa pili hapo ameandika vizuri tu,"Wakati hivi vitu vimeshaangaliwa na officer wa migration ktk ubalozi". Kwa hiyo huyo Afisa Uhamiaji wa Ubalozi ajui kazi yake?!! Au Amumwamini? Kazi ya kwanza ya Ubalozi kwa sheria za kimataifa popote duniani ni kusaidia raia wake waliopo Diaspora, ila naona watu kama nyie mna lenu jambo. Na kwa vile mmeona Marekani basi wivu, fitina, roho mbaya visivyooleweka vinwaingia moyon. Kwa ndugu zenu mnataka waangaishwe sana kwa kila kitu kwa vile wako Marekani, ambako wanaokota pesa mitaani(right)?!!. Mbona kuna Wahindi kibao wameshika Passport za KiTanzania na wengine hawajawi ata kukanyaga Bongo wala hawajui Kiswahili?!!Na wala hamsemi kitu? Vile vile kama unavyosema watoto wenu watakuhukumu kwa kosa ghani?(wacha kuongea vitu ambavyo havina uthibitsho) Tanzania iatkuwa ya mwisho kwa kila kitu kwa vile watu kama nyinyi akili zenu zimesinyaa. AMKA!, AMKA!, Amka
ReplyDeleteOfisa WA uhamiaji. Fahamu kiswahili. Passport mpya na passport za aina mpya Ni vitu viwili tofauti. Passport ikimaliza muda hutolewa mpya, pasport ikipotea unapewa mpya, ikirowa, ikichanika unapewa mpya. Aina mpya ya passport sio mada ya tangazo Hilo. Nijukumu la Serikali kutoa taarifa hiyo. Maombi Ni passport mpya. Sio passport ya aina mpya ya Tanzania. Usijichanganye na uofisa Wako. Mdau Seattle!.
ReplyDeleteHuyu mjamaa anaejiita ofisa wa uhamiaji. Anaonekana mjeuri Sana haya maelezo yake. Utadhani labda hii nchi Ni ya wazee wake. Na hii ndio kawaida ya maofisa WA idara hii. Wamejaa kibri, kejeli, dharau, ujuaji mwingi. Hii nchi sio ya ofisa wa uhamiaji Bwana. Usijitie kujua saaana!. Tanzania Ni nchi yetu sote. Jamaa ametoa wazo wewe unamjia juu! Umesoma wapi ofisa wewe jeuri na hivi ndivyo munavyoichafua nchi yetu. Alaa!
ReplyDeleteJIBU KUHUSU VYETI.
ReplyDeleteNadhani hukunielewa, kama mimi nio nje tayari nilishapata passport ninataka kubadili pasi yangu tuu, nimepeleka ubalozini tayari wamehakiki vitu vyangu vyote na wamechukuwa copy na wao ubalozi ndio wakaisili bahasha kwani nini sasa inapo fika Tanzania wanaanza kudai vitu vingine, au hawawaamini hawa wanao fanya kazi huku kwenye hizi balozi nje.
KUHUSU KENYA NA UGANDA.
Wao wenzetu wana warahisishia wenzao walio kuwa nje afisa katika balozi za nje wana badilisha pasi bila ya kupeleka tena kwenye nchi zao sio sisi ukiipeleka ubalozi unaambiwa hatujui itarudishwa lini (INAWEZA IKAWA MWEZI AU MIEZI MINNE) kwahiyo posti mwenyewe, sasa kuna wengine tuna toka vijijini hatuna ndugu Dar ninani atatusimamia.
Na ndio maana unaona hilo tangazo hivi kubadili pasi mtu mpaka tuje kama kundi mtu si iwe muda wake mwenyewe tuu.