 |
Mkurugenzi
wa Idara ya Masuala ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akiwa
na Kanali, Dkt. Edward Masalla kutoka Jeshi wa
Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) na Afika Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa Bw. Abdalla Khamis, timu
hii ndiyo iliyoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
mkutano wa Marejeo wa Mkataba wa
Silaha za Nyukilia (NP 2015)
mkutano huu ambao kwa kawaida hufanyika
kwa wiki nne umemalizika pasipo wajumbe kufikia mabakubaliano ya pamoja ya
baadhi ya vipengere muhimu.
|
 |
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy katika mkutano uliokuwa
ukijadili ajenda ya tathmini na
ufuatiliaji wa utekelezaji wa ajenda na
malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2013
mkutano ambao pia ulipitisha mada zitakazojadiliwa wakati wa
Mkutano Kisiasa wa Ngazi ya Juu wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali
watakapokutana mwezi septemba
ambapo wanatarajiwa kupitisha
ajenda na malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015. Aliyeketi nyuma ya Balozi Mushy ni Dkt. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa
ESRF. Anayeonekana nyuma kabisa ni
Bw. S. Shilla Afisa Mkuu wa
Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
|

Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ulioshirikia majadiliano kuhusu tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji
wa malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015 kutoka kushoto ni Bw. Ahmed Makame Haji, kutoka Tume ya Mipango
Zanzibar, Bi. Salma Ali Kimara Tume ya
Mipango Zanzibar na Bw. Senya Robert Tuni kutoka Tume ya Mipango Tanzania Bara.
 |
Sehemu
ya wajumbe wa Nchi wanachama zilizoshiriki katika mkutano wa Majadiliano kuhusu eneo la tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa ajenda
na malengo ya maendeleo endelevu
baada ya 2015. Mkutano huo wa wiki moja
umemalizika mwishoni wa juma hapa makao makuu ya umoja wa mataifa.
|
 |
Jaji
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Othman Chande ambaye yupo hapa
Umoja wa Mataifa kwa kazi maalum
akiwa na Kutoka kulia, Mkurugenzi wa DMC. Balozi Celestine
Mushy, Dr. Tausi Akida na Mdau Kutoka
Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...