Mwezi Mei tarehe 9, mwaka 2015, Tanzania imeandika historia nyingine baada ya kufanya Tiba ya moyo bila ya kufanya upasuaji kwa kuziba matundu yaliyoko kwenye moyo kwa kutumia “kifaa maalum” bila kufungua kifua kama ilivyozoeleka. Tiba hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini kupitia Idara ya Tiba na Upasuaji Moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 9 hadi 16 Mei, mwaka huu. Madaktari hawa wamekuja kupitia taasisi ya Al Mutanda Islami Trust ya Uingereza. Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto amesema jumla ya wagonjwa zaidi ya 20 wanatarajiwa kupatiwa tiba hii.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto kwake ni Prof. Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 8 hadi 16 Mei, mwaka huu. Aliyepo mwisho kulia ni Sheikh Said Ahmed Abri ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kiislam la hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation na shirika hili ndilo lililoratibu timu hii ya madaktari kuja kutoa huduma.
Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua kifua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2015

    Hii ni hatua nzuri ya maendeleo kwetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...