41Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.

Na Andrew Chale, Modewji blog
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti habari za sekta ya madini hapa nchini.

Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi.

Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi.

“Awali kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya madini,”alisema.

Alisema chombo hicho kilianza kutoa ripoti za ufuatiliaji wa sekta za Serikali kwa makini na fedha zinazolipwa. Alisema Ripoti ya nne ambayo ni ya mwaka 2014 inaonyesha kwamba mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tofauti na ripoti ya kwanza iliyokuwa na hitilafu ya Dola milioni 30.

Alisema mafanikio ya utaratibu huo umesaidia taasisi za Serikali kuhakikisha kwamba kila fedha inayotoka au kulipwa inakuwa ya maandishi ili kuwa na taarifa sahihi.
1Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...