.jpg)
Katika taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael Bundala amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa nchini Burundi.
TFF imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli hii ni mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF unafuatilia ili kujua ni hatua gani zichukuliwe.
Jukumu la TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si vinginevyo.
TFF inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na baraka katika nchi yao.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...