Kiongozi wa kikundi cha vijana 40 cha Wajenzi Isoso, Wilayani Kishapu akisoma risala kwa Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya (wa pili kushoto walioketi) mara baada ya Meneja huyo kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Bi. Jane Mutagurwa ambaye alimhakikishia ushiriki makini wa Halmashauri hiyo katika kuwasaidia vijana kazi, mtaji na maeneo endelevu ya kufanyia kazi yao ya kufytaua matofali yanayofungamana. Aliishukuru NHC kwa msaada wa mashine kwa Halmashauri hiyo ambazo zimewapa vijana ajira.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Festo Kang’ombe mara baada ya kufanya mazungumzo naye ya kuhamasisha Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC ya kuytatulia matofali yanayofungamana.
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwa katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga maarufu kwa ajili ya vijana wa Juakali wanaotengeneza matofali ya kufinyanga na kuchoma, ambapo aliendesha zoezi la kukinyang’anya mashine iliyotolewa na NHC kama msaada kikundi cha vijana cha Amanias katika Manispaa hiyo baada ya kugundua kuwa kikundi hicho kimeacha kutumia mashine hiyo na kujiunga na kazi za juakali za kutengeneza matofali ya udongo wa kufinyanga.
Wakufunzi wa VETA Shinyanga wakiwa eneo la Kata ya Usanda wakimueleza Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya namna wanavyoshiriki kurekebisha hitilafu ndogondogo zinazojitokeza katika mashine za vijana za kufytatua matofali yanayofungamana alipokagua vikundi vya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
HABARI ZAIDI INGIA HAPA
HABARI ZAIDI INGIA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...