Nianze mada hii kwa kurudia pongezi kwa rafiki yangu Bwana Joe, Kwa kuongezewa nguvu na Nchi yake ya Marekani. Tayari taarifa rasmi ya hili nimeiandikia, na inaweza kusomeka zaidi kwa “KUBOFYA HAPA”. Bwana Joe amekua na imani inayofanana sana na yangu kwa muda mrefu ya kua uhalifu mtandao ni mbio za sakafuni endapo hapatakua na ushirikiano thabiti.

Kume kua na hoja nyingi kutoka mataifa mbali mbali juu ya kusua sua katika ushirikiano unao vuka mipaka huku uhalifu mtandao kutotambua mipaka iliyopo katika mataifa yetu. Uhalifu mtandao umeendelea kufanyika huku ukivuka mipaka na athari kuendelea kushika kasi ya aina yake hivi sasa.

Nategemewa kuangazia changamoto kadhaa tulizo nazo katika bara la Afrika na nini kifanyike katika hotuba yangu kwa wataalam mbali mbali wa usalama mitandao baadae mwezi huu jijini Johannesburg ambapo changamoto kubwa iliyoafikiwa na wanausalama kutokea maeneo yote duniani ni kukosekana kwa ushirikiano wa dhati na endelevu katika kupambana na uhalifu mtandao.

Hili limekua ni tatizo zaidi nchini Tanzania kwani hata ushirikiano wa ndani umekua ukiyumba sana baina ya vitengo mbali mbali vinavyo husiana na usalama mitandao nchini licha ya kua na malengo yananyofanana ya kutokomeza uhalifu mitandao. Kuna kila haja ya kujiangalia zaidi kwenye hili hasa kwa sasa tunapo hitaji zaidi kua na mipango pamoja na mikakati madhubuti ya kuweza kufikia malengo ainishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...