Ushahidi wa upande wa Utetezi wa mshtakiwa wa pili, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuendelea kusikilizwa na kesho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya leo mwenyekiti wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji John Utamwa kuwa udhudu wa kikazi.

Jaji Utamwa na Jaji Samu Rumanyika  walianza kusikiliza kesi hiyo wakiwa Mahakimu Wakazi Wakuu kabla ya kupanda na kuwa Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania, ambao kwa sasa wako, Kanda ya Tabora.

Kesi hiyo iliahirishwa leo na jopo la mahakimu wawili Rumanyika na Hakimu Mkazi Mkuu, Saul Kinemela.

Pande zote mbili ziliridhia sababu hiyo na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa utetezi wa Mshtakiwa wa pili Yona, hapo kesho.

Washtakiwa wengine ni,  Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja wote wanakabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.

Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...