Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.
Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya anga nao hawakuwa nyuma na mabango yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...