Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa barani Africa wamekutana  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.

Wakuu hao ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa barani Afrika AUABC iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za Afrika ambapo mwenyekiti wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema kuwa wanatarajia kwa mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa ndani ya bara hili. 
Amesema kuwa kiwango kikubwa wanaangalia jinsi gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii kwa maana ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu za kiafrika.

Pamoja na hayo amesema kuwa tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni mfumo uliopo ambao unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo alisisistiza kwa wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa. Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa.
SAM_2509Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa kutoka Ghana Mh.Daniel Batidam akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2498Makamu Mwenyekiti bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa Mh.Florince Ziyambi kutoka Zimbabwe.
SAM_2522
Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...