Kampuni
ya Simu Tanzania(TTCL) kuwapatia wananchi waishio vijijini zaidi ya
Laki Moja mawasiliano ya Simu ifikapo mwaka 2016. Jumla USD 3.3 (sawa na
Bilioni 6.8 Tsh) zitatumika kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye
kata 41 zenye vijiji 41 kupitia ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote(UCSAF) ikiwa ni awamu ya 2B.
Kata
hizo ni pamoja; Oljoro –Arusha, Olmotonyi- Arusha, Olorieni – Arusha,
Chikola- Dodoma, Mpalanga- Dodoma, Farkwa-Dodoma, Iduo-Dodoma,
Masagalu-Tanga, Mazinde- Tanga , Mpale-Tanga, Misalai-Tanga, Ivaeny-
Tanga, Kashisha-Tanga, Kashisha-Tanga, Arri-Manyara, Ayasanda-Manyara,
Sigino-Manyara, Lengatei-Manyara, Bashay- Manyara, Buhendangabo-
Kagera, Nyakato-Kagera, Ihembe- Kagera, Mwandu- Mwanza, Kiloleli-
Simiyu, Itinje-Simiyu, Isanzu-Tabora, Neruma- Mara, Rigicha- Mara,
Bwanga-Geita, Kasenga-Geita, Lumuli-Iringa, Kihesa-Iringa, Namichiga-
Lindi, Galula-Mbeya, Luwalaje- Mbeya, Mbangala-Mbeya,Namkukwe- Mbeya,
Kajunjumele- Mbeya, Kapele- Mbeya Mdandu-Njombe, Liparamba-Ruvuma.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akizungumza
na wadau wa makampuni ya simu pamoja na wananchi waliohudhuria uwekaji
wa saini wa kupeleka mawasiliano vijijini.
Katibu
Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Patrick
Makungu akitoa hotuba katika hafla ya uwekaji wa mikataba ya kupeleka
mawasiliano ya simu vijijini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr. Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani kwa niaba ya Makampuni ya Simu, baada ya makampuni hayo kushinda zabuni ya kupeleka mawasiliano kwenye jumla ya kata 117.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr. Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani kwa niaba ya Makampuni ya Simu, baada ya makampuni hayo kushinda zabuni ya kupeleka mawasiliano kwenye jumla ya kata 117.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...