Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WANAWAKE wametakiwa kujiunga katika taasisi za fedha ambazo zinaainisha mikopo ya wajasiriamali hiyo itasaidia wanawake kujikwamua na umasikini.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Sophia Simba wakati wa uzinduzi wa mpango Fanikisha Plus wa wajasirimali unaondeshwa na benki ya Equity iliyofanyika leo katika ukumbi JB,Belmote jijini Dar es Salaam.
Sophia amesema wanawake umefika wakati kutumia fursa ambazo taasisi za fedha zenye mikakati ya kumkomboa mwanamke kiuchumi kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
“Wanawake umefika wakati wa kupata elimu ya vitu mbalimbli vinavyoendelea vya jinsi ya kuweza kujikwamua kiuchumi na sio kukaa katika luninga na kuangalia tamthilia”amesema Sophia.
Amesema katika mipango ya Umoja wa Afrika wa wameanisha jinsi ya kuweza kumasaidia mwanamke wa Afrika kumkwamua kiuchumi kwa kutoa elimu ya kuweza kujitambua hivyo wanaweza kuendesha miradi mbalimbali.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na watoto Mhe. Sophoa Simba, akizungumza na Wajasialiamali mbalimbali kuhusiana na kujiinua kiuchumi katika ukumbi wa JB belomente jijiji Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na Watoto Me. Sophia Simba, akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Bodi ya wanawake wafanyabiashara Tanzania Anna Matinde katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Equity Josef Iha.
Baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria katika warsha iliyofanyika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakaingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...