Zaidi ya watumiaji milioni 13 wa mtandao wa simu za mkononi kuanzia leo wataweza kuperuzi internet inayofikia MB100 kwa masaa mawili bure kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 2 asubuhi kutokana na ofa inayojulikana kama 
"Good Morning Tanzania" inayotolewa na Vodacom Tanzania.


Promosheni hii imeanzishwa kutokana na kuonenakana kuwepo kwa mahitaji makubwa ya matumizi ya data katika kupata  taarifa kupitia mtandao wa intaneti.Vodacom Tanzania siku zote imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma zinazoendana na matakwa ya wateja wake na kuwarahisishia maisha katika nyanja ya elimu,afya,Kilimo,burudani,huduma za kibenki na huduma nyinginezo  za kurahisisha biashara mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii leo,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni hiyo Kelvin Twissa amesema “Kupitia promosheni hii ya ”Good Morning Tanzania” Vodacom tutawaunganisha wateja wetu na sehemu nyingine za dunia bure kila siku.Ofa hii  inawawezesha wateja wetu kufanya shughuli zao mapema bure kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na marafiki,kupata habari mbalimbali za kitaifa na kimataifa na matumizi mengineyo mengi yanayoweza kufanyika kupitia kwenye mtandao wa internet.
Promosheni ya ”Good Morning Tanzania”imeadaliwa mahususi kukidhi matakwa ya wateja wa Vodacom ili kuwarahisishia maisha na watanzania wametakiwa kujiunga na familia ya Vodacom  waweze kutumia  fursa hii kupata wakipendacho kupitia teknolojia ya simu  za mkononi.
Ili kupata huduma hii mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga namba *149*01# ambapo atapata maelekezo zaidi na kuanza kupakua na kuperuzi intaneti na kuweza kupata kwa urahisi anachohitaji akiwa ametulia nyumbani kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...