Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina
Kombani, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ( kati kati) akisisitiza jambo.
Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe ( kushoto ) akiwa na mwezeshaji wa mafunzi, Patrick Ngwila.
Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, ameitaka Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii nchini kuelekeza nguvu zao vijijini kwenye idadi kubwa ya wananchi na wazalishaji wa mali wanaohitaji huduma
zao badala ya kung’ang’ania mijini pekee.
Kombani
alitoa
changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku nne yaliyoanza Mei 25
hadi kufikia 28, 2015 mjini Morogoro ya kuwajengea uwezo na ufahamu
wafanyakazi
wanaunda Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) kutoka katika
mifuko ya
Hifadhi ya jamii ya PPF,NSSF,LAPF,GEPF,NHIF na ZSSF.
Hata hivyo alisema, mifuko hiyo imekuwa ikikimbilia kutafuta
wanachama katika maeneo ya mijini na kushindwa kubuni mbinu mbadala za
kuwafikia wananchi wengi wanaoishi vijijini.
Kwa mujibu wa Waziri
huyo kuwa, dhana iliyojengeka kutoka kwa Mifuko hiyo kuwa vijijini hakuna watu
wenye vipato sasa imepitwa na wakati kwa kuwa wananchi wanaishi vijijini ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara
ndogo ndogo ambao wanaouwezo mkubwa wa
kuchangia mifuko hiyo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...