Akiwa njiani kwenda Hanoi, Vietnam, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ( Kazi
Maalum),Profesa Mark Mwandosya, amekutana na Edson Arantes do
Nascimento (Pelé) mwanamichezo maarufu sana duniani. Pelé atatimiza umri
wa miaka 75 ifikapo tarahe 23 Oktoba,2015. Katika uhai wake, Pelé
aliweza kuingiza magoli 1283 katika michezo ya ushindani wa mpira wa
miguu.
Pelé aliichezea timu yake klabu ya Santos, Brazil kuanzia mwaka
1956 mpaka mwaka 1974.Baada ya kustaafu alijiunga na klabu ya New York
Cosmos kwa muda mfupi kuanzia mwaka 1974 mpaka 1977. Pelé ametajwa kuwa
mmoja wa watu maarufu zaidi duniani na hakika mwanasoka maarufu kuliko
wote karne ya 20.
Waziri Mwandosya alimshukuru Pelé kwa kuwa mfano bora
katika mwenendo, maisha, ubunifu,na uongozi katika tasnia ya michezo na
alimtakia afya njema na maisha marefu. Amewahi kuwa Waziri wa
Michezo,Brazil. Katika picha ni Waziri Mwandosya, kulia;Pelé,katikati;na Mama Lucy Mwandosya, kushoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...