Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameendelea na ziara ya kikazi jimboni kwake huku Makundi mbalimbali yaliendelea kumuunga Mkono na kumshawishi achukue fomu ya Ubunge kwa kipindi kijacho.

Katika ziara yake ya kichama amekagua kazi zinazotanywa na kikundi cha wakina mama wafinyanga vyungu, wakinamama wajasiriamali wauza kokoto na walima bustani.

Aidha amezindua Shina la ushindi ambalo wakinamama wafinyanga vyungu ndiyo wanachama wa Shina hilo, Katika kuunga Mkono vikundi hivyo mbunge amewachangia pump ya kumwagilia na Fedha vyote kwa pamoja vinafikia sh 2,800,000.

Wakitoa ujumbe kupitia nyimbo walimtaka mbunge wao muda ukifika achukue fomu kwani wameridhishwa na kazi nzuri alizozifanya kijijini hapo ikiwepo huduma za jamii.

Akihutubia katika mkutano huo aliwapongeza kwa kujiunga katika vikundi na mafanikio yanaonekana. Amewapongeza kwa bidha nzuri za majiko, vyungu na upatikanaji wa kokoto kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Amewahakikishia ushirikiano wa dhati na atachukua fomu kutetea nafasi yake mara muda utakapofika.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akilakiwa na wananchi wa jimbo lake hilo.

Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika moja ya mikutano na wananchi wa jimbo lake hilo.
Akipokea zawadi ya kuku.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikabidhi mashine ya kuvutia maji kwa wananchi wa moja ya kijiji katika Jimbo lake la Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...