TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema watu 152 watafikishwa mahakamani mkoani Njombe kutokana na kujiandikisha mara mbili katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration Kit’ (BVR).

Aidha, imeeleza kuwa kata 130 zimeongezeka kutokana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kufanya mabadiliko ya kiutawala katika kata, vijiji,vitongoji na Mitaa hivyo kulazimu NEC kuhairisha kwa wiki moja uandikishaji wa daftari uliokuwa ukianza jana kwa baadhi ya mikoa.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Sisti Cariah alisema hayo jana wakati akielezea kuahirishwa kwa wiki moja uandikishaji hadi Juni 16 mwaka huu kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara.

Akizungumzia suala la watu kujiandikisha mara mbili, alisema katika mkoa wa Njombe ambao Daftari hilo liko tayari na wiki ijayo litawekwa wazi kwa siku tano na kisha kufanyiwa marekebisho kwa siku moja na wamebaini watu 152 waliojiandikisha mara mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2015

    danganya toto hio , hizi ni njama kujidai kama vile NEC inafanya kazi yake kwa uhakika kumbe kiini macho ,wanaandikishwa watu ambao hawastahiki kwa maelfu , mtadanganya wasio na maarifa na mbumbumbu , UKAWA amkeni msilale usingizi kazi bado kubwa sanaaaaa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2015

    HOW IS IT POSSIBLE, THAT IS WHAT WE CALL CONSPIRACY BETWEEN THE CREW OF REGISRA AND THE VOTERS, IT DONE DELIBERATELY.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2015

    Tufuate sheria tujiandikishe mara moja ukijiandikisha mara mbili kompyuta itakugundua. Sheria zimewekwa kutuwezesha kufuata taratibu tunapozikiuka tunakaribisha mkanganyiko na kujiumiza wenye. Sasa mtu anaandikisha mara mbili ili iweje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...