Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu za washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 kukamilika, takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata mshindi.

akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki, Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.

Jaji huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za juu kutoka mikoa tofautitofauti.

Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania  Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote  watatembelewa maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.

Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie  L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang  Manyara,  Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani  Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida, Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini, Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera  Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48)  Kilombero Morogoro, Stella Fabian  Masulya (42) Ukerewe Mwanza,  Regina Kapili Stephano (19)  Mpanda  Katavi, Rehema Daniel  Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.
Jopo la Majaji, Kutoka Kulia ni Zephaniah Muggitu wa Digital Consulting Ltd, Jairos Mahenge Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi  Oxfam akikaribisha majaji kwa ajili ya kutaja majina ya washindi watakao ingia shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...