Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo Leonard Thadeo akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa
Airtel Rising Star msimu wa tano. Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini
Dar es Salaam leo 17th June,2015
Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
michezo Leonard Thadeo akiwa alama ya uzinduzi wa kampeni ya " Its
Now" yenye kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao katika Nyanja
mbalimbali kama technologia, michezo na muziki. Wakishuhudia ni Rais
wa TFF Jamali Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi
Beatrice Singano Malya (kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la
vijana Bwana Ayoub Nyenzi
Wachezaji wa Airtel Rising Star 2013 ambao sasa wanachezea timu ya
wanawake ya Taifa Twiga Stars wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
uzinduzi wa program ya Airtel Rising Stars ya msimu wa 5 iliyofanyika
katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania
Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema kampuni ya Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka minne iliyopita.
"Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua
vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu
za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20", alisema Singano.
Kumbukumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake
imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo
madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17.
Singano pia ametangaza kampuni ya Airtel kuingia mkataba na nahodha wa
Ivory Coast na kiungo wa Manchester City Yaya Toure katika kampeni
mpya iitwayo "It's Now" yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani
Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha
mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka
17.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...