Na woinde shizza ,Arusha
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja  amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo  ya taifa.

Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo  itakayoleta  mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.

Akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza taifa hili” Alisema Isanja

Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni wa heshima katika mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa misingi ya ukabila na udini na kutowachagua  kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.

Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa  Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na linategemewa kukamilika nchini kote  ili kukamilisha uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja (wapili kushoto) akiwa katika mahafali ya chuo cha Bibilia kinachomilikiwa na kanisa hilo.watatu kushoto ni Mgeni Rasmi Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...