Mkutano wa 39 wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirikia hilo jijini Roma hapo tarehe 6 -13 Juni, 2015 umemchagua tena Balozi Wilfred Joseph Ngirwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la FAO (Independent Chairperson of the FAO Council - ICC) kwa kipindi cha miaka miwili (2015-2017).
Katika Mkutano huo ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri (NW) wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mhe. Godfrey Weston Zambi (Mb), Balozi Ngirwa alikuwa mgombea pekee kama ilivyokuwa Juni, 2013 aliposhinda kwa kishindo pia na kushika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka miwili (2013 - 2015).
Kuchaguliwa kwa balozi Ngirwa ni mwendelezo wa
mafanikio ya diplomasia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na umakini wa
Serikali katika kuteua wagombea wa nafasi kama hizo za kimataifa wenye sifa,
uzoefu na umahiri usiomashaka katika nyanja husika. Hakika hayo ni miongoni mwa
mambo yaliyo mpamba siku zote Balozi Ngirwa pamoja na sifa na uzalendo wake kama
Mtanzania. Aidha, kwa ufahamu wake wa kina wa maboresho yanayoendelea
kutekelezwa katika FAO, umahiri na uwezo wake mkubwa wa kuongoza vikao na
kupata mwafaka (consensus), ukiwemo mwafaka kwa mara ya kwanza wa viwango vya
Bajeti, vimewezesha Baraza la FAO kufikia mafanikio mengi na mkubwa chini ya
uenyekiti wake katika awamu yake ya kwanza ya miaka miwili (2013 – 2015).
Tunamtakia Balozi Ngirwa, na Baraza la FAO, mafanikio makubwa zaidi katika
kipindi cha mwaka 2015 – 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...