Watanzania wameshauriwa kuzidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umasikini. 
Katibu Mtendaji wa Bazara la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa amewaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa wakati serikali inafanya juhudi kuwawezesha wananchi, ni muhimu wananchi pia wakaongeza juhudi katika shughuli zao za kiuchumi. 
“Tuko katika njia nzuri kufikia uchumi wa kati, lakini inabidi kuongeza kasi ya kazi na ufanisi,” alifafanua. 
Alisema Tanzania itafikia baadhi ya vigezo mwakani lakini ili kufikia uchumi wa kati wa hali ya juu kama zilivyo nchi za bara la Asia bidii zaidi itahitajika,” alisema. 
Pato la Mtanzania kwa mwaka sasa ni wastani wa dola za Kimarekani 1038 na ili kufikia kiwango kilichofikiwa na nchi za Asia itatakiwa kufikia pato la wastani wa dola 3,000. “Kukamilisha azma hii lazima tufikie uchumi wa viwanda,” alisema. 
Alisema baraza linaendelea kufanya kazi ya kuwaendeleza watanzania kuweza kuinua vipato kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Posta kuhakikisha vikundi vilivyo katika sekta isiyo rasmi vinaingizwa katika mfumo rasmi kama kuwa na akaunti benki na kutambuliwa na mfumo rasmi wa vyombo vya fedha nchini. 
Akitoa mfano alisema inakadiriwa kuwa Tanzania ina vikundi vingi vya vicoba vilivyo na jumla ya Tshs Trilioni Moja katika mfumo usio rasmi. Pia alisema inakadiriwa kuna vijana milioni moja wameajiriwa kama madreva bodaboda, na kwamba mkakati uliopo ni kuwapa elimu na kuwawezesha. 
Alisistiza kuwa katika kufanikisha hilo wana mpango wa kuwawezesha kwa kuanza na mikoa ya Dar es Salaam,Kigoma, Dodoma na baadaye maeneo mengine nchini. Alisema wanafanya kazi na Sekta Binafsi nchini (TPSF) kuhakikisha sekta hiyo inakuwa shindani na inazalisha bidhaa nyingi na bora. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi amesema benki yake itaendelea kushirikiana na Baraza hilo kuhakikisha watanzania hasa vijana wanainuka kivipato. 
“Huduma za kibenki ni muhimu katika harakati za kupambana na umasikini na sisi kama benki tunaunga mkono baraza hili,”alisema. Alisema benki yao hadi sasa ina zaidi ya akaunti 320 za vikoba zenye thamani ya zaidi ya Tshs 300 milioni ambazo zipo sehemu salama kuliko ilivyokuwa awali.
 Katibu Mtendaji wa Bazara la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi.Beng’i Issa (kushoto) akizindua akaunti ya vikundi visivyo rasmi ya Benki ya Posta nchini jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Mikopo wa benki hiyo, Bw. Henry Bwogi (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.
Katibu Mtendaji wa Bazara la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi.Beng’i Issa (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi baada ya kuzindua akaunti ya vikundi visivyo rasmi ya Benki ya Posta nchini jana jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...