Keki iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Watoto Halima Revocatus (7) na Filex Mustach (6) wakikata keki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika yaliyofanyika katika tawi la Benki ya CRDB Mlimani City jijini Dar es Salaam, Benki ya CRDB uadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu ni Timiza Ndoto Yako na Junior Jumbo Account. Nyuma ya watoto hao ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Angela Mnamba akiwasaidia watoto kukata keki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika ambayo uadhimishwa kila ifikapo Juni 16 ya kila mwaka ambapo benki hiyo hufanya maadhimisho hayo kwa kusherehekea na watoto pamoja na wateja.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango akimlisha keki mmoja wa watoto katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Afrika iliyoadhimishwa katika tawi hilo kwa kuwashirikisha watoto pamoja na wateja.
Mtoto Miguel Karim Milton akiwa na furaha baada ya kupokea zawadi kutoka Benki ya CRDB tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...