Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Molel (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa madawati 30 kwa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlingotini, Wediel Besha, yaliyotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Bagamoyo, Pwani jana.
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Molel (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakati akikabidhi msaada wa madawati 30 yaliyotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Bagamoyo mkoani Pwani.
Meneja Mafunzo wa Benki ya NBC, John Nyaindi (kulia ) akikabidhi baadhi ya madawati kwa mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Mjaka Chamwamba wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakifurahia baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati kutoka NBC na Mkuu wa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Flora Molel (kulia).
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakipozi kwa picha na Mkuu wa Rasilimali Watu wa NBC Flora Molel (nyuma kulia) katika hafla hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya shule, Mjaka Chamwamba (kushoto), na Mwalimu Mkuu wa shule ya Mlingotini, Wediel Besha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...