Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback (kulia) mara tu alipowasili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo. (Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker
Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.
Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara tu baada Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin W. Mkapa kuzindua rasmi huduma mpya ya NMB Mastercard. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...