Design Mpya ya Tshirts
Bei 25,000/= per peace
Designer ; Mike Mwakatundu
Shop ; Kitaa Wear
Kwa Mawasiliano
Email; mwakatundu.m@gmail.com
+255 754 310 202
+255 713 292 212
NB Unaletewa mpaka Nyumbani/Ofisini
Kama upo interested na bidhaa nyingine zaidi hizo hapo chini tembelea blog yetu www.dukaletu.blogspot.com
Ili kuwajua watengenezaji waagizaji wa bidhaa mbalimbali, mahoteli, usafiri , address sahihi za watu mbalimbali maarufu hapa nchini tembelea blog yetu www.tanzaniasocialmedia.blogspot.com
Nimeupenda huo ubunifu. Nitanunua nikiziona madukani
ReplyDeleteDalili za ukabila. Wana maadili munaona? au fofofo.
ReplyDeleteMdau wa pili acha ndoto mbaya [jinamizi],ktk hiphop za bongo tuna artist[s] wanaojitambulisha kupitia maeneo wanayotoka kama mfalme wa moro Afande sele, mwamba wa kaskazini Joh MAKINI, mfalme wa mbeya Izzo B, mwana wa darisalama Kiba, Top in dar TID au mnyama, yupo na yule wa Tandale anayetuwakilisha akina sie, haya ukitoka nje ya mipaka ya bara USA, kuna westcoast, east coast, pia kuna wale wa vitongoji Mfano ndani ya New york city wapo wa Brooklyn,Bronx, Queens, Long beach na hawa wote wana Tshirt zao ni kawaida tu,haya ukija Sweden nilipo hivi sasa kila mkoa na vitongoji vinatengeneza Tshirt zenye kuonesha au kutaja majina ya eneo husika ni kawaida tu, Tena umenikumbusha nina Tshirt niliyoinunua Venice italy......sasa huu ukabila wa kwako kaa nao ndani mwenyewe watu wanafikiri vingine sasa huu ni wakati wa kuthubutu kibiashara zaidi, najua wasiwasi wako eti kuna uchaguzi....hahahahahaha
ReplyDeleteMdau wa pili hapo juu nakuunga mkono Tanzania ni nchi changa na siyo USA ya Bronx, Long Beach hivyo wadau wote wakiwemo wafanyibiashara wazingatie Tanzania ina umri wa miaka 50 tu na bado tunakazi ngumu ya kujenga ''taifa'' moja lisilojibainisha na ukabila.
ReplyDeleteANONY WA TATU unahusudu mambo ya kuiga. Huko marekani na huko Sweden unakodai unaishi uelewa wa watu si sawa na uelewa wa watanzania. Zingatia pia kuwa Wala uelewa wao sio bora kuliko uelewa wa watanzania mpaka tuwaige. ANONY WA PILI katoa maoni yake akizingatia kulinda umoja wala hakutaja mambo ya uchaguzi. Kwanza wewe unaishi Sweden huo uchaguzi wa Tanzania unaushabikia wa nini, tuachie sisi tunaoishi na kuvumilia changamoto za nchi nyetu tujali na kuchagua viongozi wetu wenyewe, wewe chagua huko huko Sweden au Marekani.
ReplyDeleteUlivyo ndumilakuwili umedai kuwa "Yule wa Tandale anaetuwakilisha akina sisi" Wewe unaishi Sweden unawakilishwaje na mtu wa Tandale kama sio ngebe. Sidharau mtu hapa, lakini hao wasanii wote uliowataja hapo juu ufahamu wao juu ya dunia inavyokwenda ni kama wako. POLE.
Madau hapo juu ulivyofafanua ni sawa. Wasanii wanajitambulisha kutoka maeneo waliyotoka tangu enzi na enzi.
ReplyDeleteKuvaa T-shirt imeandikikwa Kilimanjaro au Tabora ni sawa; lakini sio sawa kabisa na kuvaa imeandikwa Chagga, au Nyamwezi...huko ni kushabikia ukabila. Chaga au Nyamwezi ni makabila, sio sehemu.
Usiandike makabila, andika miji, vitongoji n.k.
Mdau wa 3, ata iwe East au West Cost au tandale ata iwe A town hii yote ni ukabila...Tanzania yetu ni moja tu haina ukabila wala udini.
ReplyDeleteHongera sana lakini naomba sana iwe kwa mikoa yote ikiwezekana kwa wilaya na vitongoji maafurafu au bila kukosa mitaa! Nipo DSM asili yangu Chalinze wenyewe tunaiita CHOX a.k.a CHAD waulize wote hapa town watakwambia au watu wote wa malori na mabasi ya mikoani watakwambia, tutoleeni kitu na sisi tujivunie kwetu!
ReplyDeleteSi vibaya kwa mtanzania kujitambulisha kabila au upande wa tanzania aliotokea lakini itakua ni vibaya sana kwa mtanzania kuona kabila au upande wa tanzania aliotokea ndio bora zaidi kuliko makabila na pande nyingine za tanzania
ReplyDelete