Msafara wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Makongoro Nyerere umepata ajali wilayani Kasulu mkoani kigoma mapema leo hii.

Msafara huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini, ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.

Watu waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.

tutaendelea kuwajuza zaidi juu tukio hilo
Gari lililopata ajali katika msafara wa Mgombea urais, Charles Makongoro Nyerere lililokuwa limebeba wasaidizi wake.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya kasulu wakishangaa ajali ya gari la wasaidizi wa mgombea urais kupitia CCM, Charles Makongoro Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2015

    Poleni mliopata ajali.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2015

    HEE GUYS, EASY AND SLOW DOWN, YOU WILL BE FINE, DON'T WORRY.
    HAITAKUWA NA MAANA MKIFA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...