Christian Bella akijimwaga jukwaani. |
Masaa machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka katika Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) alipagawisha wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na kundi zima la Malaika Band. Christian Bela alitarajiwa na wadau wa muziki nchini kuwa angebeba tunzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz kutamba sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini, lakini kama kawaida ya tunzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na kampuni ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila mwaka huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tunzo hiyo ya wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali Kiba. Onesho hilo lilifanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
Bella akifanya yake jukwaani. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...