Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari juu ya tuzo waliopata Dubai katika udhibiti wa Nishati iliofanyika Ofisi za EWURA, leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mhandisi wa Umeme EWURA, Anastas Mbawalla.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi akionyesha kitabu cha kinachofafanua masuala ya mikataba katika sekta ya Nishati ambacho Mtaalam wa Mhandisi wa Umeme, Anastas Mbawalla (kushoto)alishiriki katika kuandika kitabu hicho.
Mhandisi wa Umeme wa EWURA, Anastas Mbawalla akizungumza na waandishi wa habari juu alivyoshiriki katika kuandika kitabu cha masuala ya mikataba ya nishati iliofanyika leo katika ofisi za EWURA jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu EWURA, Felix Ngamlagosi.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.GLOBU YA JAMII)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imeibuka mshindi wa mashindano ya Tuzo ya Mdhibiti Bora wa mwaka wa Nishati 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Felix Ngamlagosi amesema kuwa tuzo hiyo imetolewa Juni 8 mwaka huu kwenye uzinduzi wa sherehe za 17 za Mkutano Mkuu wa Kila mwaka wa Nishati wa Afrika uliofanyika Dubai.
Ngamlagosi amesema kuibuka kwa EWURA katika Tuzo za Nishati inalenga kuwatambua wale wote ambao wametoa mchango kwa maendeleo ya soko la nishati barani Afrika.
“Ushindi wa Tuzo ya Udhibiti Bora wa mwaka wa nishati 2015 imetambua mchango wetu wa udhibiti kutokana na huduma tunayotoa kwenye malengo ya kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya nishati kutokana na mahitaji”amesema Ngamlagosi.
Amesema tuzo hiyo inaifanya Tanzania sasa itambulike Kimataifa kwa kuwa na taasisi thabiti ya uhakika ya udhibiti wa sekta nishati na maji ,ambalo ni jambo la muhimu kwa nchi kuendelea kuimarisha imani ya wawekezaji ambayo inatakiwa sana katika kuvutia mitaji binafsi kwenye sekta ya nishati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...