
Mwanadada Nunu Ntshingila ndiye atakae ongoza ofisi
hiyo itakayo jikita katika kutafuta njia mbali mbali za kuongeza ushirikiano na
wafanya biashara wa barani humo.
Tayari watumiaji wa facebook barani Afrika ni milioni
120, ofisi hiyo mpya inalenga kuongeza idadi ya watumiaji wake nchini Kenya,
Nigeria na Afrika Kusini.
Nunu Ntshingila ndiye mkurugenzi mkuu wa ofisi hiyo
ambae amesema kuwa mkakati wa kupanua uwekezaji wao hasa katika matangazo ni
mipango mikubwa ya kutanua biashara pamoja na bara la Ulaya na maeneo ya
Mashariki ya Kati.
Barani Afrika kuna mtumiaji mmoja kati ya watano wa
intanenti na inatarajiwa idadi hiyo kukua mara mbili zaidi kwa watumiaji wa
simu za mkononi ifikapo mwaka 2020.
Asilimia 80% ya wanao tumia facebook ni wale wenye
kupata huduma hiyo kupitia simu zao za mikoni.
Facebook anasema pia ina mipango madhubuti ya kuongeza
wateja kutoka nchi za Senegal, Ivory Coast, Ghana, Tanzania, Rwanda, Uganda,
Zambia, Msumbiji na Ethiopia ili kufikia malengo yake.
Kwa msaada wa mtandao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...